Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan kurejea kuishi Uingereza

Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan kurejea kuishi Uingereza
Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan kurejea kuishi Uingereza

Wanawafalme hao walitikisa vyombo vya habari duniani baada ya kujiondoa kwenye ufalme
WANANDOA hao wanatarajiwa kuondoka Marekani baadaye mwezi huu na kuhamia katika makazi binafsi, yasiyo rasmi ya kifalme, nje ya mji wa London.

Taarifa hiyo imeripotiwa na gazeti la Daily Telegraph na The Sun.

Watoto wao, Archie mwenye umri wa miaka saba na Lilibet mwenye miaka mitano, wamesajiliwa kuanza masomo katika shule moja nchini Uingereza, mwezi Septemba mwaka huu.

Mfalme Charles amearifiwa kuhusu mpango huo siku ya Jumapili.

Kwa sasa, hakuna mipango ya Mwanamfalme Harry au Meghan, kurejea katika majukumu yao ya kifalme.

Wawili hao walihama nchini Uingereza na kujiondoa katika majukumu yao ya kifalme mwanzoni mwa mwaka wa 2020 na kuhamia Jimbo la California, Machi mwaka huo.

Tangu wakati huo, uhusiano wao na familia ya kifalme ya Uingereza ilikuwa na misukosuko.

Hata hivyo, ziara ya Harry na Meghan ya mwezi Julai ya kumtembelea Mfalme Charles na Malkia Camilla, ilionekana kuwa hatua muhimu katika kuboresha uhusiano wao.

Related Posts