Kipindi nilipokuwa shule, nilijulikana kama mwanafunzi “anayejaribu lakini hafanikiwi.” Kila muhula ulipofika mwisho, majina yaliposomwa darasani, langu halikuwahi kukaribia orodha ya wanaofanya vizuri.
Walimu waliniona kama aliyekata tamaa. Wenzangu walinicheka, wengine wakinionea huruma. Kila niliporudi nyumbani, nilikuwa na mzigo mkubwa moyoni hisia kwamba nimewaangusha wale waliokuwa wananiamini.
Nilijitahidi kusoma. Nilikaa masaa mengi usiku, lakini kichwa kilionekana kizito, kumbukumbu ikikataa kukaa. Kila jaribio lilionekana kuishia pale pale.
Nilianza kujiuliza kama tatizo lilikuwa mimi, au kulikuwa na kitu kingine kinachonizuia. Kicheko cha watu kilinifanya nijione mdogo, na siku moja nilijikuta nikisema, “labda shule sio kwa ajili yangu.” Soma zaidi hapa
