Kusoma kwa bidii, kupata shahada ya kiwango cha juu, na kuwa na vigezo vyote vinavyohitajika sokoni halafu kila unapoomba fursa unakataliwa ni mtihani mzito unaoweza kumfanya mtu yeyote aanze kujitilia shaka na kuteseka kisaikolojia.
Kwa zaidi ya miaka mitatu, nilikuwa nikitaabika sana kutafuta ajira au ufadhili wa masomo ya juu ughaibuni. Nilialikwa kwenye usaili mara saba tofauti katika makampuni na mashirika makubwa ya kimataifa. SOMA ZAIDI.
