Nilianza biashara yangu ya kuuza bidhaa ndogo mtandaoni kwa matumaini makubwa. Nilikuwa na ndoto ya kujitegemea na kuendesha biashara yangu bila kuomba msaada kwa mtu yeyote.
Hata hivyo, mambo hayakuwa kama nilivyotarajia. Nilikaa miezi mingi bila kupata hata mteja mmoja. Nilikuwa napoteza matumaini taratibu, nikijiuliza labda hii biashara haikunifaa.
Kila siku nilichapisha matangazo kwenye mitandao ya kijamii, lakini watu hawakuwa wanavutiwa. Wengine waliuliza bei, kisha kimya. Nilijaribu punguzo, ofa, hata matangazo kwa malipo, lakini bado hakukuwa na mafanikio.
Wakati mwingine nilihisi kama mtandao unanipuuza kabisa. Nilianza kufikiria kuacha, hasa baada ya kutumia akiba yangu yote bila kupata faida yoyote. Soma zaidi hapa
