Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Paul Christian Makonda kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akichukua nafasi ya Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum).
Uteuzi huo umefanyika hii leo Januari 8, 2026 ambapo kabla ya uteuzi huu, Makonda alikuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo.
