Nature

Rais Samia Amteua Dr Mapana na Jenifa Omolo Makatibu Maendeleo ya Vijana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Nov 20,2025 amemteua Jenifa Christian Omolo kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana na kabla ya uteuzi huo Omolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha.

Pia Dkt. Samia amemteua Dkt. Kedmon Elisha Mapana kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana awali alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa na uapisho wa Viongozi hawa wawili utafanyika Ikulu Chamwino, Dodoma, tarehe 21 Novemba 2025 saa 8:00 mchana.

Related Posts