Rais wa klabu ya Petro de Luanda Tomas Faria ameweka ahadi ya kutoa zawadi ya dola za Marekani 350,000 sawa na takribani Sh milioni 902 endapo timu yake itafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Simba SC.
Ahadi hiyo imetolewa ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wachezaji wake kuelekea mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa leo dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania.
Kwa sasa Kundi D linaongozwa na Stade Malien wenye pointi 8 wakifuatiwa na Esperance wenye pointi 6 huku Petro Atletico ikiwa na pointi 5 na Simba SC ikiwa na pointi 4.
Matokeo ya mchezo huu yanatajwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kuamua hatma ya timu zitakazofuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo ya kimataifa…
