Refa wa Fainali AFCON Kuchezesha Mechi ya Yanga na JS Kabylie Ligi ya Mabingwa Africa

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) linatarajiwa kumteua mwamuzi wa kimataifa kutoka DR Congo 🇨🇩 Jean-Jacques Ndala kuchezesha mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Young Africans SC na JS Kabylie.

Mchezo huo wa kihistoria unapangwa kuchezwa tarehe 15 Februari katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar .

Ndala ni mwamuzi mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika, akiwa ndiye aliyechezesha fainali ya AFCON 2025, jambo linaloonesha kiwangoratuo chake cha juu na imani kubwa aliyonayo CAF.

Inaripotiwa pia kuwa atawasili akiwa na kikosi kilekile cha waamuzi aliokifanya kazi kwenye fainali hiyo ya AFCON.

Kwa uzito wa mchezo huu—ambao unaamua hatma ya kufuzu hatua inayofuata—uteuzi wa Ndala unaongeza hadhi, umakini na mvuto mkubwa kwenye pambano hili la moto.

Mashabiki wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla wanatarajia uchezeshaji wa haki, weledi na nidhamu ya juu katika mechi hii ya maamuzi

Related Posts