Shaffih Dauda “Simba Imedhulumiwa, Yanga Imebahatika”

 

Shaffih Dauda "Simba Imedhulumiwa, Yanga Imebahatika"
Shaffih Dauda “Simba Imedhulumiwa, Yanga Imebahatika”

Simba ilikua timu bora kiwanjani Steve Barker alimuuliza maswali mengi magumu ya kiufundi Kocha wa Yanga Pedro Goncalves.

Mechi inaisha ‘Man of the Match’ ni kipa wa Yanga-Djigui Diara, hii inakupa tafsiri kuwa kuna moto ulikua umewashwa na Simba mithili ya makombora ya USA kwa Iran.

Unaiangalia Simba ambayo imetengeneza nafasi nyingi za wazi, na kuisumbua defence ya Yanga, unakubali na kusema, YES✅

Unaiangalia Simba ambayo ilizuia vyema, chini ya Majemedari wa vita DE REUCK na TOURE, unatingisha kichwa na kusema YES✅

Unaingalia Simba ambayo ilishinda mapambano mengi uwanjani, Juu walikua vizuri, Chini walitakata, unaishia kukubali mbinu za Kocha Steve Barker, Unasema Yes✅

Hapa naiongelea Simba iliyokua bora kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho. Ni Simba ambayo hakuna alietegemea anaweza kuwa na mikazo ya kibabe namna hii

Simba ilikua ni timu iliyostahili points 03 kwenye mechi hii kama isingekua dhulma ya mshika kibendera

Hii ndio mechi ambayo Yanga ameondoka na point 1 yenye bahati kubwa sana kwake, Simba kadhulumiwa ndani ya Mwezi Mtukufu!

NB: Karia alisema atamfungulia Mashtaka refa ambae ataharibu hii Derby. Hvyo tujiandae kwenda kusikiliza kesi Mahakamani.

Related Posts