Shirika la Reli Tanzania Lakanusha UJENZI wa SGR Kusimama

Shirika la Reli Tanzania limewataka wananchi kutupilia mbali upotoshaji wa makusud i unaofanywa na baadhi ya watu kuwa mradi wa SGR umesimama na kwamba tayari Shirika limeshapata mkandarasi wa ujenzi wa ujenzi wa vipande mpaka Mwanza na pia Tabora mpaka Kigoma kwa maana ya Uvinza mpaka Musongati Burundi.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Machibya Shiwa, ametoa tamko hilo katika banda la maonesho la TRC katika maonesho ya kimataifa ya 49 ya biashara maaarufu kama Sabasaba, ambapo pia anewahakikishia Watanzania kuwa mradi huo utakamilika kabla ya 2030 kama yalivyo maono ya Rais Samia kwakuwa rasilimali fedha zipo.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi mkuu huyo wa TRC, ametoa wito kwa Watanzania hususani watumiaji wa reli kutoa mrejesho katika kipindi cha mwaka mmoja wa uendeshaji wa SGR, ulioanza Juni 2024.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *