Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtengua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi George Simbachawene ambapo nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Patrobas Katambi.
Utenguzi huo umefanyika hii leo Januari 8, 2026 kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu ambapo itakumbukwa kwamba Simbachawene aliteuliwa kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani mwezi Disemba mwaka jana baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika oktoba 29.
