
Sura ya Mtoto wa Jux na Priscilla Ojo Yazua Mjadala Mzito Mitandaoni
Siku tatu baada ya mwanamuziki wa Bongo Flava, Juma Jux, na mkewe Priscilla Ojo (Priscy) kufichua sura ya mtoto wao, Prince Rakeem Mkambala, mjadala mkubwa umeibuka mtandaoni kuhusu nani hasa mtoto huyo amefanana naye. Picha hizo ziliwekwa wazi Agosti 24, 2026, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa Rakeem, baada ya wazazi wake kuficha sura yake kwa kipindi chote hicho.
Baada ya pongezi za siku ya kuzaliwa, mashabiki wamegawanyika katika makundi tofauti: wapo wanaodai mtoto huyo amebeba muundo wa uso wa baba yake Jux, huku wengine wakiona amefanana zaidi na bibi yake (mama wa Jux) au mjomba wake, Mkambala JR. Licha ya hisia hizo za mashabiki, familia haijatoa kauli yoyote, huku ikitambuliwa kuwa mwonekano wa Rakeem utaendelea kubadilika kadiri anavyokua.
