Nature

TANESCO yazindua mita janja kupunguza changamoto za token

Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter) yenye lengo la kuboresha na kumrahisishia mteja kufanya manunuzi ya umeme moja kwa moja ikiwa ni mageuzi makubwa ya teknolojia yanayofanywa na TANESCO katika kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wateja.

Waziri wa Nishati amezindua Mita janja hizo Disemba 05, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa sekta ya nishati na watendaji wa TANESCO.

Amesema Mita hizo mpya zinamwezesha mteja kupata umeme mara moja baada ya kufanya manunuzi ya token bila kutumia kifaa cha ziada cha kuingiza namba (CIU), hatua inayolenga kupunguza changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mfumo wa zamani.

“Leo tunajivunia hatua kubwa ya kihistoria zilifanywa na TANESCO ikiwa ni moja ya kampuni za umma inayofanya vizuri katika utoaji huduma kwa wateja nchini. Mita janja inaleta mapinduzi makubwa katika namna Shirika hili linavyofanya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato,” ameeleza Mhe. Ndejembi.

Ameongeza kuwa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wateja wakati wa kuingiza token ndiyo zimeisukuma Serikali kufanya mageuzi ya kiteknolojia.

Related Posts