Tinubu Ashinda Uteuzi wa APC Kugombea Urais Nigeria 2027

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, amepata rasmi tiketi ya chama tawala cha All Progressives Congress (APC) kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Tinubu alipata ushindi huo baada ya kura za mchujo za chama hicho zilizofanyika nchini kote, akimshinda mpinzani wake pekee Stanley Osifo kwa kupata zaidi ya kura milioni 10.9, kwa mujibu wa viongozi wa APC.

Akizungumza mjini Abuja baada ya ushindi huo, Tinubu alisema ataendelea kusukuma mbele mageuzi ya kiuchumi pamoja na miradi ya maendeleo ya taifa.

Rais huyo alisema serikali yake itaendelea kuweka mkazo kwenye:

Ukuaji wa uchumi
Viwanda
Usalama wa nishati
Maendeleo ya miundombinu
Usalama wa chakula
Tangu aingie madarakani, utawala wa Tinubu umeanzisha mageuzi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo kuondoa ruzuku ya mafuta na kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa ubadilishaji fedha za kigeni, hatua ambazo serikali yake imesema zinalenga kuimarisha uchumi na kuongeza imani kwa wawekezaji.

Aidha, Tinubu alieleza kuwa serikali yake imeendelea kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo usafiri, umeme, makazi, umwagiliaji na huduma za kidijitali.

Related Posts