
Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS kimeomba kikutana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dharura ili kuweza kuwasilisha kwake naoni ya wadau mbalimbali juu ya changamoto ambazo zinapaswa kutatuliwa kabla ya uchaguzi ili kuliwezesha taifa kuingia kwenye uchaguzi likiwa na amani na haki iweze kutendeka katika uchaguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 26, 2025 jijini Dar es Salaam, Rais wa TLS Boniface Mwabukusi amesema “TLS imewasiliana na Ofisi ya Mhe. Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasilisha maazimio ya wadau”
ALSO READ | Baba Levo Amtishia Nyau Zitto Kabwe “Saa Tano na Nusu Nitakuwa Nimeshachukua Jimbo Kigoma Mjini”
Mwabukusi ameeleza kuwa mazungumzo hayo na Rais yatazingatia kutoa ushauri wa hatua za haraka kuchukuliwa ili kurudisha imani ya wananchi na kuhakikisha uchaguzi unakuwa shirikishi, shindani na wenye uhalali wa kisiasa.
Ameongeza kuwa hadi hivi sasa hawajapata majibu kutoka ofisi ya Rais huku akisisitiza umuhimu wa serikali TLS kuwasilisha maoni hayo”tunayo nafasi ya kusimama imara kama taifa kwa kusikilizana na kuelewana kwenye masuala muhimu ya kitaifa kama suala la uchaguzi mkuu”
TLS Kimeomba kikutana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Dharura
ALSO READ | TLS: Tutashirikiana na Poleple Kuhusu”Mifumo ya NIDA, INEC na CCM

