Trump na Rais wa Iran Wasaini Makubaliano ya Kusitisha Mvutano

Trump na Rais wa Iran Wasaini Makubaliano ya Kusitisha Mvutano
Trump na Rais wa Iran Wasaini Makubaliano ya Kusitisha Mvutano

Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian wamesaini Hati ya Makubaliano ya Maelewano (MOU) inayolenga kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili na kuweka msingi wa ushirikiano katika masuala ya usalama, diplomasia na utulivu wa kikanda.

Serikali za Iran na Marekani zimethibitisha kusainiwa kwa makubaliano hayo, huku maafisa wa pande zote wakisisitiza kuwa hatua inayofuata ni utekelezaji wa ahadi zilizowekwa kwenye hati hiyo.
Ingawa maudhui yote hayajawekwa wazi, makubaliano hayo yanatajwa kugusa masuala ya mpango wa nyuklia wa Iran, vikwazo vya kiuchumi na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.

Wachambuzi wanaamini hatua hiyo inaweza kufungua ukurasa mpya wa mahusiano kati ya Tehran na Washington, huku pia ikitarajiwa kuwa na athari chanya katika utulivu wa soko la mafuta duniani.

Related Posts