Nature

Tumeibiwa Vitu vya Bilioni 2 Kanisa la Gwajima

‎Askofu Baraka Thomas Tege wa Kanisa la ufufuo na uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ametao taarifa ya jumla kuhusu upotevu wa mali uliobainika baada ya kufanya tathmini ya mali na vifaa vingine vilivyopotea tangu kanisa hilo lifungiwe na kuweka chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi.

‎Akisoma taarifa hiyo Novemba 30, 2025, mbele ya Waumini wa kanisa hilo pamoja na Vyombo vya Habari vilivyokuwepo, amesema thamani ya vitu vyote vilivyopotea na kuharibiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 2 na milioni saba.

‎”Milango ya kawaida mitatu imevunjwa, Meza ile ya Baba imevunjwa zile droo zimefunguliwa vifaa kule havipo, documents hazipo, na sefu ya kuhifadhia fedha zetu kama nilivyosema, imevunjwa vunjwa kabisa, Hizi sio mali za siku moja, ni mali ambazo zimekusanywa kwa miaka 30, thamani yake ni bilioni 2, milioni saba, laki sita sabini na sita na miatano” amesema Askofu Tege.

‎Tathmini ya upotevu na uharibifu wa mali za kanisa hilo lililopo Ubungo jijini Dar es salaam, ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maagizo ya Mkuu wa wilaya ya Ubungo Albert Msando alipofika kanisani hapo kwaajili ya kuruhusu kuendelea kwa shughuli za kikanisa.

Related Posts