Tundu Lissu Ahoji Kinga ya Mashahidi: Asema Rais na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi Wanaweza Kuitwa Mahakamani

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, leo Agosti 21, 2026, ameiambia Mahakama Kuu kuwa hakuna kiongozi au afisa yeyote wa Serikali aliye juu ya sheria kiasi cha kutoitwa kutoa ushahidi mahakamani.

Akiwasilisha hoja zake kuhusu mashahidi anaotaka waitwe kwenye kesi inayomkabili, Lissu amefafanua kuwa hata Rais anaweza kupelekewa wito wa mahakama kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Binafsi wa Rais. Ingawa amekiri kuwa mahakama haiwezi kutoa hati ya kumkamata Rais au kumlazimisha kufika, amesisitiza kuwa uamuzi wa kuuheshimu wito huo utabaki mikononi mwa Rais mwenyewe.

Lissu ameongeza kuwa viongozi wastaafu kama Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu wastaafu, pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama—akiwemo Mkuu wa Majeshi (CDF), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkurugenzi wa DCI, na Mkurugenzi wa Ujasusi—wote wanaweza kuitwa na hata kupelekewa hati ya kukamatwa kisheria wakikaidi wito.

Akiomba mahakama kulinda haki yake ya msingi ya kuwaita mashahidi hao, Lissu amesema: “Kama kwenye kesi kubwa kama hii mahakama haiwezi kupeleka wito, basi sijui itaonekanaje. Lindeni haki yangu ili kuweka haki katika kesi na uadilifu.”

Related Posts