Kesi ya uhaini No. 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu inaendelea sasa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Jumatatu Februari 09.2026
Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru inaendelea leo kufuatia kuahirishwa mara ya mwisho Novemba 12.2025
Kesi hiyo inaendelea leo kwaajili ya upande wa Jamhuri kujibu mapingamizi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na mshtakiwa (Tundu Lissu) ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo,
Hata hivyo, kabla upande wa Jamhuri haujaanza kujibu mapingamizi hayo, Tundu Lissu aliieleza Mahakama kuwa ana hoja kadhaa za kuwasilisha Mahakamani hapo zinazohusu mwenendo wa Magereza na kesi yake kwa ujumla wake, hivyo kuona hayaendi, miongoni mwa mambo aliyoyawasilisha ni lile linalohusu uendeshaji wa kesi
Tundu Lissu anasema katika mwenendo wa kesi hiyo tangu mwanzo haki zake zimekiukwa kwa kiasi kikubwa lakini yote si hayajafanywa na Majaji au Mawakili wa Serikali wanaohusika na kesi hiyo
Amesema ametimiza siku 307 tangu awekwe mahabusu ambapo ni sawa na miezi 10, au wiki 44, lakini kwa muda wote huo kesi yake imesikilizwa kwa siku 14 tu (leo siku ya 15), na kwamba kuna siku 88 za ukimya kuanzia Novemba 12.2025 kesi hiyo ilipoahirishwa mara ya mwisho hadi leo ilipotajwa tena, yaasiku zote hizo 88 kesi haijasikilizwa kabisa
“Muda wote huo nipo gerezani hakuna kinachoendelea, waheshimiwa Majaji tukumbuke msemo wetu mama kuwa haki inayocheleweshwa ni haki iliyokiukukwa, Mahakama zinaelekezwa na Katiba yetu kwamba ziendeshe mashauri kwa namna ambayo haitachelewesha haki” -Lissu
Katika maelezo yake, mshtakiwa (Tundu Lissu) ambaye anajitetea mwenyewe ameelekeza lawama zake kwa wapangaji wa ratiba ya kesi hiyo, ambapo amesema utaratibu wa kuendesha kwa njia ya vikao (session) badala yake kushauri kwamba ni vyema kesi hiyo ikaendeshwa kwa njia ya kawaida
Amesema Jaji Mkuu ndio mwenye mamlaka ya kuamua shauri gani liendeshwe kwa njia gani, na kwamba njia hiyo ya ‘session’ imepingwa na kukosolewa kwa muda mrefu na wadau wa Mahakama, katika eneo hilo amerejea kile kilichoelezwa kwenye ripoti
