
Aliyekuwa Mbunge wa Tanga Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ummy Mwalimu, ameondoshwa kwenye orodha ya wagombea walioteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Badala yake, CCM imempitisha Kassim Mbaraka kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo hilo, hatua inayoashiria mabadiliko ya kiuongozi ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu.

