Taarifa kutoka Yanga zinaeleza kwamba mazungumzo na Kocha Rulani Mokwena yanaendelea vizuri, huku kocha huyo akiendelea kutoa masharti mbalimbali, lakini changamoto kubwa ni kwamba ofa tofauti zimeendelea kumfuata tangu aachane na Wydad.

Kocha huyo anataka mambo machache ya kuboreshwa ikiwemo kutanua benchi la ufundi na kusajiliwa wachezaji anaowataka masharti ambayo mabingwa hao wa kihistoria nchini wanapambana nayo.

“Tunataka kufanya maamuzi mapema ili kocha aje kabla ya Ligi kuisha atoe mapendekezo yake ya mwisho ili maandalizi ya msimu ujao yaanze mapema.” kilisema chanzo changu ndani yake ya Yanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *