Nature

Vilabu Ligi Kuu Vyainyooshea Kidole Yanga….

Vilabu Ligi Kuu Vyainyooshea Kidole Yanga….

Wakati Yanga ikishikilia msimamo wa kutaka kulipwa fedha za zawadi ikiorodhesha Sh200 milioni baadhi ya klabu zimeigeuka zikidai haijawahi kutangazwa juu ya badiliko la zawadi za ubingwa wa michuano hiyo inayotoa mwakilishi wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabiti Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema klabu yao iliyocheza fainali mbili mfululizo zilizopita inachokijua ni kwamba zawadi za bingwa wa FA ni Sh50 milioni tangu michuano ikiwa chini ya udhamini wa Azam.

Zakazi aliongeza, hata wadhamini wapya walipoingia haikuwahi kuainishwa na TFF juu ya zawadi halisi ya michuano hiyo, zaidi ya shirikisho hilo kupanga lenyewe, hivyo wameshtushwa kusikia zawadi imeongezeka hadi Sh200 milioni.

Ofisa Habari wa Singida Singida Black Stars iliyotinga fainali za msimu huu, Hussein Massanza alisema hawajapata mabadiliko yoyote juu ya ulipwaji wa fedha za bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho na sasa wapo katika mchakato wa kufuatilia kabla ya kuvaana na Yanga

Akizungumza, Massanza alisema wanachofahamu bingwa wa michuano hiyo analipwa Sh50 milioni, lakini sasa wameshtuka na kuanza kufuatilia kujua kama kuna mabadiliko baada ya kutinga fainali.

“Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ameanza mchakato wa kufuatilia endapo tutatwaa ubingwa tutapata kiasi gani kwa sasa, lakini miaka yote tunafahamu ni Sh50 milioni hatuna mabadiliko yoyote tuliyoyapata.”

Mkuu wa Coastal Union, Omar Ayoub alisema hawana mabadiliko yoyote kuhusiana na fedha anayopokea bingwa wa mashindano. “Tulicheza hatua ya fainali kiasi kinachotambulika miaka yote ndio tulichokuwa tunakifahamu. Kwa sasa sijui bingwa anachukua bei gani kama kuna mabadiliko sisi hatuna taarifa hiyo,” alisema.

Hata hivyo, alisema kwa utaratibu wa michuano hiyo kila hatua inayoshiriki timu kuna fedha inapewa kwa ajili ya mechi husika, japo kwa zawadi halisi ya bingwa haijawahi kujulikana tangu mdhamini mpya aiingie.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *