Ajali Mbaya ya Ndege, Air India Yaanguka na Kuwaka Moto na Abiria 242
Leo Juni 12, 2025, ndege ya abiria ya Air India imeanguka na kuwaka moto muda mfupi baada ya kupaa kutoka Ahmedabad, India, ikielekea London, Uingereza. Kwa mujibu wa taarifa zilizotufukia ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 242, wakiwemo wafanyakazi 12 wa ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ikiwa na usajili namba VT-ANB na serial namba 36279. Ilianza kutumika nchini India mwezi Januari mwaka 2014, na imekuwa ikifanya safari za kimataifa kwa takriban miaka 11.
Ajali hiyo imetokea ghafla baada ya ndege kupoteza mawasiliano na mnara wa kuongozea ndege, jambo ambalo bado halijafahamika chanzo chake. Baada ya kupoteza mawasiliano, ndege hiyo ilianguka na kulipuka kwa moto mkubwa katika eneo la karibu na Ahmedabad, hali iliyosababisha taharuki kubwa kwa wakazi na familia za abiria.
Timu za dharura tayari zimefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada na kuanza shughuli za uokoaji. Hata hivyo, hadi kufikia sasa hakuna ripoti rasmi kuhusu waliojeruhiwa au kupoteza maisha, na jitihada zinaendelea ili kuokoa maisha ya abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Mashuhuda waliokuwa karibu na eneo la tukio wameripoti kuona moshi mzito na kusikia mlipuko mkubwa. Serikali ya India imeanzisha uchunguzi mara moja ili kufahamu kiini cha tukio hili la kusikitisha.
Ndege za Boeing 787-8 Dreamliner zinatambulika kwa kutumia teknolojia ya kisasa na ufanisi mkubwa wa mafuta, lakini ajali hii imeibua maswali mapya kuhusu hali ya usalama wa ndege hizo, hasa kwa zile zilizotumika kwa muda mrefu.
Kwa sasa, dunia inasubiri ripoti kamili kutoka kwa mamlaka husika nchini India, huku matumaini yakiwa juu ya kupata walionusurika. Endelea kufuatilia kwa taarifa zaidi kadri zinavyoendelea kujitokeza.
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.