Vita ya Uenyeji AFCON 2028, 2031 na 2033 Yaanza Rasmi

Vita ya Uenyeji AFCON 2028, 2031 na 2033 Yaanza Rasmi
Vita ya Uenyeji AFCON 2028, 2031 na 2033 Yaanza Rasmi

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limefungua rasmi mchakato wa kuwania uenyeji wa matoleo matatu yajayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), yatakayofanyika mwaka 2028, 2031 na 2033.

Mabadiliko hayo yamesababisha marekebisho ya ratiba ya Mashindano, ambapo matoleo ya mwaka 2032 na 2036 yameondolewa na nafasi zake kuchukuliwa na matoleo ya mwaka 2031 na 2033. Mabadiliko hayo pia yanazingatia kalenda ya kombe la Dunia la mwaka 2030.

CAF imezitaarifu nchi zote Wanachama kupitia vyama vyao vya soka, ikiziruhusu kuwasilisha maombi ya kuandaa mojawapo ya matoleo hayo, ikiwemo zile ambazo hazikushiriki katika mchakato uliopita.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa, nchi zinazotaka kuwania uenyeji zinapaswa kuwasilisha nia yao ifikapo Novemba 17, 2026, huku nyaraka kamili za maombi zikitarajiwa kuwasilishwa kabla ya Desemba 8 mwaka huu.

Hatua hiyo inalenga kuharakisha mchakato wa kupata wenyeji wa mashindano hayo na kutoa muda wa kutosha kwa maandalizi.

Related Posts