Nature
Baada ya Kukatwa CCM, Mpina Agonga Hodi ACT Wazalendo, Awagawa Wanachama

Wananchi wa Jimbo la Kisesa Wamlilia Luhaga Mpina “Hatuoni Kosa Lolote Alilofanya”

Wakati zoezi la kupiga kura za maoni likiendelea leo kwa wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwachagua wagombea wa Ubunge na Udiwani watakaokiwakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, baadhi ya wananchi wa Jimbo la Kisesa, mkoani Simiyu, wamesema wapo njia panda kufuatia jina la aliyekuwa Mbunge wao, Luhaga Mpina, kutorudishwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kwa ajili ya kuwania tena nafasi hiyo.

Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, wamesema walitarajia jina la Mpina lipitishwe, kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jimbo hilo wakati wa kipindi chake cha ubunge.

Kwa mujibu wao, wanaeleza kuwa hawaoni kosa lolote lililofanya Mbunge huyo kutoteuliwa, huku wakisisitiza kuwa bado wanamuhitaji kutokana na mafanikio aliyoyasimamia ikiwemo kuboreshwa kwa miundombinu, huduma za afya, upatikanaji wa maji safi na mengineyo.

Ikumbukwe kuwa, leo wagombea waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM wanapigiwa kura za maoni na wajumbe katika ngazi ya kata.

Awali, Julai 29, 2025, akiwa Jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, alitangaza majina ya wagombea walioteuliwa na kusisitiza kuwa mchakato huo ulikuwa wa haki, huku akiwataka wale ambao hawakupata nafasi kuwa watulivu na kuendelea kuiunga mkono CCM.

Jambo TV

Related Posts