Wananchi wa Senegal Wameanzisha Kampeni ya Kumchangia Kocha Faini

Wananchi wa Senegal wameanzisha kampeni ya kuchanga ili kulipa faini ya dola za Marekani 100,000 ($100,000) iliyopigwa kocha wao Pape Thiaw baada ya fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Morocco.

Mpaka sasa, kampeni hiyo imeshakua na zaidi ya dola za Marekani $4,300 sawa na FCFA 2,400,000, Kwa shilingi za Kitanzania ni milioni 10.9

Hata hivyo Pape Thiaw amewashukuru na amewaomba michango hiyo wapewe watu wenye uhitaji.

Related Posts