
Wolper Agusia Tabia za Kajala, Aunty Ezekiel na Irene Uwoya; Ataja “Vichwa Vigumu” vya Kundi
Staa wa Bongo Movie na mjasiriamali, Jacqueline Wolper, ameanika ukweli kuhusu tabia za mashoga zake wa karibu—Kajala Masanja, Aunty Ezekiel, na Irene Uwoya—huku akikiri kuwa yeye na Uwoya ndio “vichwa vigumu” zaidi kundi hilo.
Wolper amefunguka haya kuhusu tabia zao:
-
Kajala Masanja: Ni mpole na mwenye huruma, lakini usimzoee—ana ukali wake mambo yakiharibika.
-
Aunty Ezekiel: Mpambanaji asiyechoka, anayependa ubuyu (kufuatilia mambo), mdaku wa stori, lakini ana roho ya kipekee ya huruma.
-
Irene Uwoya: Ana hasira za karibu sana (mle wepesi wa kuwaka), lakini ana upendo mwingi na ni mtu wa ibada.
Vipi kuhusu ugomvi wao? Wolper ameweka wazi kuwa huwa wanatofautiana mara kwa mara, lakini hawaweki vinyongo. “Sisi tunasusa wote na tunarudi haraka,” alisema. Pia, aliongeza kuwa yeye binafsi anapenda sana mapishi
