Huyo mwamba hapo anaitwa Taibi Lagrouni, huyu ndio alikuwa fitness coach wa @yangasc ya Miguel Gamondi,
Huyu jamaa amewahi kufundisha pale RS Berkane, watu walipigishwa jaramba mpaka wakataka kuhama 🤔🤣,
Viongozi wa RS Berkane wakamwambia “mjomba, shikilia hapo hapo, sema nao😁, Kweli, matunda yalionekana na RS Berkane wakachukua ubingwa wa CAFCC,
Baada ya kuja Young Africans aliifanya vyema sana, ile Yanga iliyomtoa jasho @sundownsfc home & away ilikuwa ni physicality iliyotengenezwa na @taibilagrouni ,
Fitness ya Yanga Sc ilikuwa juu sana, wachezaji walikuwa na uwezo wa kucheza dakika 120 bila kukata pumzi 🙌
Baada ya ujio wa Sead Ramovic, yeye alimkataa Taibi hivyo kuja na kocha wake wa fitness, Adnan Behlulovic.
Yanga hawakuachana na Taibi bali walimbadilishia kitengo tu, Taibi alianza ku deal na wachezaji ambao wanafanya recovery ya injury huku akiwapa program za mazoezi @yangasc_princess
na Yanga Sc ya vijana (U-20),
Baada ya Ramovic kuondoka, kocha mpya @miloudhamdiofficial alimrejesha tena Taibi Lagrouni kama fitness coach, na kazi yake ilionekana kama ilivyokuwa awali.l 🤝
Mwishoni mwa msimu mkataba wake uliisha, Yanga wakaamua kutoendelea nae na kumleta Mokalia Chyna ambaye alikuja na mzee wa Minuno 🧐
🙆Nimemkumbuka tu rafiki yangu Taibi, Kipenzi cha Wana Yanga kwa muda wote 🙌
By Directorjozk

