Klabu ya Yanga imelimwa adhabu ya million tano (5,000,000) kwa kosa la shabiki wake kuonyesha kitendo cha kishirikina kwenye mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Coastal Union (0-1).
Ripoti inaeleza kuwa shabiki wa klabu hiyo alienda kutoa kitu kwenye lango la Coastal Union kwenye mchezo ambao Yanga walikuwa wageni uliopigwa kwenye dimba la Jamhuri Jijini Dodoma.
