Zuchu, ametumia ukurasa wake wa Instagram kufichua siri kuwa wazo la wimbo mpya wa msanii wa Nigeria, Rema, linafanana kabisa na wazo walilobuni yeye na mtayarishaji wa muziki wa Singeli kutoka Tanzania.
Kupitia ujumbe wake kwenye InstaStory, Zuchu amesema kuwa alipokuwa akifanya kazi ya kutengeneza wimbo na mtayarishaji huyo, walikuja na wazo ambalo baadaye lilionekana kufanana kwa karibu na kazi ya Rema.

“Nimeamini mimi na producer mkali sana wa Singeli tuna wimbo ndani,” aliandika Zuchu, akisisitiza kuwa walikuwa wamejipanga kutoa kazi yenye ubunifu wa hali ya juu.
Lakini kilichoshangaza zaidi ni pale alipodokeza kuhusu tukio la kugongana mawazo na Rema:
“Rema alitoa ‘kelebu’, tukakutana kuulizana mbona tumegongana wazo,” aliandika kwa mshangao. Hata hivyo, alihakikisha kuwa walikuwa mbele ya muda kwa kusema:
“Kama mtayarishaji mwenza, najua wazo letu lilikuwa la kwetu kabisa.”
Zuchu pia alielezea imani yake kwa watayarishaji wa muziki wa Tanzania, akiamini kuwa wanavuka mipaka ya ubunifu na wako tayari kushindana na wakali wa dunia.

“Nikasema basi, Tanzania ina vipaji sana kiasi kwamba tunaweza kuwaza sawa na waliotutangulia.”
Katika hitimisho lake lililojaa matumaini, Zuchu aliandika:
“Ninajivunia sana watayarishaji wetu. Tunakua. Muda wetu unakaribia…”
Kauli hizi zinavutia tuliozliotafsiri kuwa ni ujumbe wa harakati mpya katika muziki wa Tanzania, harakati za kuamini ubunifu wa ndani na kushirikiana kitaalam.

