TANZIA; Muasisi wa Chadema Afariki Dunia

Usiku wa Januari 19 2026 Chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema imepata pigo baada ya kifo cha muasisi na Moja ya nguzo Kuu ya Chama hicho Mzee Edwin Mtei Aliyefariki Akiwa Tengeru jijini Arusha. Katika taarifa hiyo ambayo imetoka kwa Makamu mwenyekiti wa Chama hicho John Heche familia imethibitisha msiba huo.

John Heche kupitia page yake ya Instagram alithibitisha taarifa hizo huku akisema Chama itatoa utaratibu wake. Heche aliandika ” Tumepokea taarifa kua muasisi Wa Chama chetu Mzee Edwin Mtei amefariki usiku wa Januari 19 2026. Chama chetu kitatoa taarifa za msiba kesho Asubuhi”.

Heche aliongeza kua ” Tunachukua nafasi hii kutoa pole sana kwa familia ya Mzee Mtei ndugu jamaa na marafiki, Chadema umepoteza Moja ya nguzo imara sana ya Chama chetu Tunamuenzi Mzee Mtei kwa mema yote aliyofanya kwa Nchi na Chama Chetu Pumzika kwa amani Mzee Mtei” Aliandika Makamu huyo wa Chadema.

Edwin Mtei alizaliwa 12.71932 mkoani Kilimanjaro alikuwa moja kati ya wasomi Wachache ambao walifanikiwa kusoma katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kutokana na uwezo mkubwa darasani na hasa katika kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha mkubwa.

Mwaka 1967 aliteuliwa kua Gavana wa BOT na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na huko alifanya mageuzi makubwa ya Nchi kwa kutengeneza wataalamu wengi wa Uchumi kupitia mafunzo ya ziada na ushauri wa kiuchumi kwa Rais.

Kubwa kuliko nje ya Chadema kwa Mzee Mtei ni Mkopo aliochukua wa Dola 50000 mwaka 1977 wakati wa vita vya Uganda, wakati ambao Uchumi wa Tanzania ukiwa katika Hali mbaya kutokana na vita ile. Ila historia hazijawahi kuandika Msaada wake huo.

Related Posts