MREMBO wa filamu za Bongo Movie, Nana Dollz, ameibua mjadala mzito mitandaoni baada ya kuweka wazi mabadiliko ya msimamo wake kuhusu mwanaume anayemtaka katika maisha yake ya kimapenzi.
Nana Dollz amesema kuwa kwa muda mrefu alikuwa akitamani mwanaume aliyemzidi kipato, lakini sasa ameamua kubadili kabisa mtazamo huo.
Kwa mujibu wa msanii huyo, suala la wanawake kutaka wanaume wenye pesa limekuwa gumzo kubwa katika jamii, jambo lililomsukuma kufanya uamuzi mpya.
“Hii ishu ya kutaka mwanaume aliyenizidi kipato, yaani mwenye hela, imekuwa kubwa sana.
“Sasa hivi mimi nimesema nimeona; kuanzia leo sitaki mwanaume mwenye pesa, nataka mwanaume ambaye hana kitu kabisa,” amesema Nana Dollz.
Kauli hiyo imezua maoni tofauti miongoni mwa mashabiki na wadau wa burudani, ambapo baadhi wameipongeza kama mtazamo wa unyenyekevu, huku wengine wakiitafsiri kama kauli ya utani au yenye ujumbe wa siri.
