Tundu Lissu Alalamika Kutopewa Chakula, Kesi Yahairishwa

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, jopo la Majaji watatu (3) wanaosikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu wamelazimika kuahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 15, hiyo ni baada ya mshtakiwa ambaye anajitetea mwenyewe kulalamikia kutopewa chakula

Awali kesi hiyo iliahirishwa kwa muda wa karibu Saa 2 ili kutoa nafasi ya watu kupata chakula, na kutoa nafasi kwa upande wa Jamhuri kumleta shahidi wa mwingine baada ya yule wa awali (P5) kukamilisha kutoa ushahidi wake

Baada ya Mahakama kurejea, mshtakiwa Tundu Lissu aliieleza Mahakama kuwa yuko tayari kuendelea na kesi hiyo ingawa hajapatiwa chakula cha mchana kutoka kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza

Lissu amesema kwa mujibu wa taratibu mahabusu (walioko gerezani) wanajigharamia chakula, na yeye ana Hela yake iliyoshikiliwa na Magereza, lakini ameshangazwa kuona hajapatiwa chakula.

Related Posts