Tangu Lionel Messi aliposajiliwa na Inter Miami, klabu hiyo imekuwa na mabadiliko makubwa ya kifedha na kitaaluma.
Mapato ya klabu yameongezeka kutoka dola milioni 56 (Sh 134.4 bilioni), yaliyokuwa karibu na kiwango cha chini katika Ligi Kuu ya Marekani (MLS), hadi kufikia dola milioni 200 (Sh 480 bilion), hali iliyosababisha Inter Miami kuwa klabu yenye mapato makubwa zaidi ligi ya Marekani.
Mbali na ongezeko la kifedha, Messi ameiletea timu taji na ushindi wa mashindano, jambo lililoifanya Inter Miami kuwa klabu yenye thamani kubwa zaidi MLS, ikiwa imetathiminiwa kufikia dola bilioni 1.35 (Sh 3.24trilioni).
Uchunguzi huu unaonesha jinsi uhamisho wa nyota wa kimataifa unavyoweza kubadilisha hali ya kifedha, umaarufu na ushindani wa klabu katika soka la Marekani
