Steve Barker Amgomea Oura Kuondoka Simba SC: Ofa ya Dola Milioni 1 Yakataliwa?

Steve Barker Amgomea Oura Kuondoka Simba SC: Ofa ya Dola Milioni 1 Yakataliwa?
Steve Barker Amgomea Oura Kuondoka Simba SC: Ofa ya Dola Milioni 1 Yakataliwa?

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka msimamo mkali kuwa bado anamhitaji kiungo mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Anicet Oura, katika mipango yake ya msimu mpya wa mashindano, licha ya nyota huyo kuendelea kuwaniwa kwa kasi na klabu kadhaa za ughaibuni.

Oura amekuwa kivutio kikubwa kwa timu mbalimbali za Ulaya, zikiwemo Bursaspor ya Uturuki, Vikingur Reykjavik ya Iceland, na DAC 1904 ya Slovakia, ambazo zote zimeonyesha nia ya kumsajili.

Hata hivyo, miamba ya soka ya Uturuki, Bursaspor, imeongeza presha kubwa katika mbio hizo baada ya kuwasilisha ofa nono inayokadiriwa kufikia Dola milioni moja za Marekani (zaidi ya Shilingi bilioni 2.6 za Kitanzania).

Licha ya thamani hiyo kubwa ya kifedha, Kocha Barker hajaonyesha utayari wowote wa kumuachia kirahisi mchezaji huyo. Barker anaiamini sana safu yake ya ushambuliaji na anaona uwezo wa Oura wa kutengeneza nafasi, ubunifu, na nguvu kwenye eneo la mbele utakuwa nguzo kuu ya Simba katika kampeni za msimu ujao.

Kujitokeza kwa ofa hiyo kubwa kunaiweka bodi na uongozi wa Simba SC kwenye mtihani mzito wa kufanya uamuzi:

Kuheshimu msimamo wa kocha Steve Barker na kumbakisha Oura ili kuimarisha kikosi.

Au kuchukua fursa ya kifedha na kumuuza mchezaji huyo kwa faida kubwa ya klabu.

Kwa sasa, hatma ya Anicet Oura inabaki kuwa njiapanda huku mashabiki wa Msimbazi wakisubiri kwa hamu kuona uamuzi wa mwisho wa uongozi wa Simba SC.

Related Posts