Andrew Mountbatten Kuondolewa Katika Orodha ya Urithi wa Ufalme Uingereza Kisa Skendo ya Jeffrey Epstein.

Serikali ya Uingereza inafikiria kutunga sheria ya kumuondoa Andrew Mountbatten-Windsor katika orodha ya urithi wa ufalme.

Waziri wa Ulinzi Luke Pollard aliiambia BBC kuwa hatua hiyo, ambayo itamzuia Andrew kuwa Mfalme ni “jambo sahihi kufanya”, bila kujali matokeo ya uchunguzi wa polisi.

Kwa sasa Andrew, ndugu wa Mfalme, bado ni wa nane katika orodha ya kurithi kiti cha ufalme licha ya kuvuliwa hadhi na majukumu ya kifalme mwaka jana, kufuatia shinikizo kubwa kuhusu uhusiano na mfadhili wake na mtu aliyedaiwa kujihusisha na watoto kimapenzi, Jeffrey Epstein.

Alikamatwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma na kuachiwa chini ya uchunguzi, akikanusha makosa yote.

Related Posts