Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Octoba 29 Yaongezewa Muda Kukamilisha Majukumu

Tume ya Kuchunguza Matukio yaliyojitokeza Oktoba 29, 2025 imeongezewa Siku 42 na kutakiwa kukamilisha majukumu yao Aprili 3, 2026 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume hiyo Februari 20, 2026.

Ikumbukwe tume ilikuwa ikamilishe ripoti kabla au siku ya Februari 20, 2026, ila kutokana na sababu 5 walizotoa, ikiwemo wingi wa taarifa, pamoja na ulazima wa kutumia Wataalam na kutoa fursa kwa wadau wachache muhimu ambao kwa sababu mbalimbali bado hawajafika mbele ya Tume, licha ya kupelekewa mialiko zaidi ya mara moja.

Pia, tume hiyo imetoa wito kwa baadhi ya viongozi wa dini, viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika yasiyo ya Kiserikali na watu binafsi ambao waliopokea mialiko na Tume lakini bado hawajafika mbele ya Tume kutumia fursa hii kufika au kuwasiliana na Tume kutoa mchango wao katika uchunguzi unaoendelea.

Related Posts