Allan Okello Aweka Rekodi ya Kipekee: Atwaa Mataji Mawili ya Ligi Kuu Ndani ya Msimu Mmoja!

Allan Okello Aweka Rekodi ya Kipekee: Atwaa Mataji Mawili ya Ligi Kuu Ndani ya Msimu Mmoja!
Allan Okello Aweka Rekodi ya Kipekee: Atwaa Mataji Mawili ya Ligi Kuu Ndani ya Msimu Mmoja!

Allan Okello Aweka Rekodi ya Kipekee: Atwaa Mataji Wawili ya Ligi Kuu Ndani ya Msimu Mmoja!

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Allan Okello, ameweka rekodi ya kihistoria baada ya kufanikiwa kutwaa medali mbili za ubingwa wa Ligi Kuu katika nchi mbili tofauti ndani ya msimu mmoja wa 2025/26.

Okello alianza msimu huu nchini mwao akiichezea klabu ya Vipers SC, ambapo mchango wake mkubwa uliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uganda (UPL) na kumfanya astahili kupewa medali yake ya ubingwa. Baada ya hapo, alihamia Young Africans (Yanga SC) ya Tanzania na leo hii amehitimisha msimu kwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya NBC Premier League, na hivyo kukusanya jumla ya medali mbili za ligi tofauti ndani ya mwaka mmoja.

Katika msimu wake huu wa kwanza akiwa na jezi ya Yanga, nyota huyo amekuwa na mchango wa dhahabu. Okello amehusika moja kwa moja kwenye mabao 21 ya mabingwa hao wa kihistoria—akifunga magoli 14 na kutoa pasi za mabao (asisti) 7. Takwimu hizi zinamfanya kuwa mmoja wa nguzo kuu zilizoifikisha Yanga kwenye kilele cha mafanikio msimu huu.

Related Posts