
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulenga ( @abdallahulega ) ametangaza zawadi ya shilingi milioni 10 kwa Wanafunzi Wahandisi wanaosoma Vyuo vikuu watakaoandika andiko la kibunifu lenye kutatua changamoto na kuleta suluhu katika Wizara ya Ujenzi ikiwemo suluhu ya changamoto ya foleni katika Jiji la Dar es salaam.
Ulenga ameyasema hayo hii leo Februari 23, 2026 wakati akizungumza na Vijana Wahandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Uhandisi na Teknolojia (COET) ambapo amesema Washindi hao mbali na kiasi hicho cha fedha watapata nafasi ya kusajiliwa Kampuni ambazo zitaenda kutatua changamoto hizo.
“leo nitaweka challenge kwenu Wahandisi kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam Wanafunzi na Vyuo vingine natoa hapa donge nono kwa watakaoandika vizuri wakaleta suluhu ya mambo mambo yalivyo uweze kuwa ni chemchem ya fikra chanya ya kutatua changamoto zilizopo Nchini kwetu na ninataka niseme moja kwa moja kwamba kwa muda wote nitakaokuwa Waziri wa Ujenzi Vijana watakaoandika suluhu ya changamoto zinazotukabili tutatoa milioni 10” – Waziri Ulega
