
Melania Trump anatarajiwa kuwa Mwanamke wa kwanza kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Marekani itachukua Mamlaka ya Baraza la Usalama la Wanachama 15 kwa muda kuanzia Machi 3, Ikulu ya White House ilitangaza.
Haya yanajiri huku Rais Trump akiukosoa mara kwa mara Umoja wa Mataifa akisema chombo hicho chenye Wanachama 193 hakijafikia malengo yake, hali iliyomfanya aondoe Marekani katika baadhi ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Marekani pia inadaiwa na Umoja wa Mataifa Mabilioni ya Dola. Kufikia mapema mwezi huu, utawala wa Trump ulikuwa haujalipa malipo yake katika bajeti ya kawaida ya UN ya 2025.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya mwishoni mwa mwezi uliopita kwamba Umoja wa Mataifa unaweza kukabiliwa na mgogoro mkubwa wa kifedha ikiwa nchi zote Wanachama zitashindwa kulipa ada zao
