
Msanii na mfanyabiashara maarufu wa muziki, Diddy, anatarajiwa kuachiwa kutoka gerezani mapema zaidi ya ilivyokuwa imepangwa awali
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Rolling Stone, tovuti rasmi ya Federal Bureau of Prisons imeonyesha kuwa tarehe ya kuachiliwa kwa mwanamuziki huyo imeletwa mbele kwa zaidi ya wiki tano. Sasa anatarajiwa kuachiwa huru tarehe 25 Aprili 2028.
Anatumika Kifungo cha Miezi 50
Diddy kwa sasa anatumikia kifungo cha miezi 50 katika gereza la FCI Fort Dix, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili yanayohusiana na ukahaba.
Tangu alipowasili katika gereza hilo mwezi Oktoba, tarehe yake ya kuachiliwa imekuwa ikibadilika mara kadhaa. Hapo awali ilikuwa imepangwa kuwa ni Mei 8, 2028, kisha ikasogezwa hadi Juni 4, 2028 mwezi Novemba 2025, kabla ya sasa kurekebishwa tena hadi Aprili 25, 2028.
Mabadiliko haya yanaashiria uwezekano wa kuhitimisha kifungo chake mapema zaidi kuliko ilivyotarajiwa awali.
