Rais Samia Amuasili Mtoto Mchanga Aliyetelekezwa Tabora

Rais Samia Amuasili Mtoto Mchanga Aliyetelekezwa Tabora
Rais Samia Amuasili Mtoto Mchanga Aliyetelekezwa Tabora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan amemuasili mtoto mchanga wa kike leo, Jumatano Machi 11.2026, katika makazi yake, Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma

Mtoto huyo aliyepewa jina la Grace Samia Suluhu alitelekezwa Mjini Nzega, Mkoani Tabora, na amekabidhiwa kwa Rais Dkt. Samia na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mtoto huyo, Mkuu wa Wilaya Tukai amesema mtoto huyo aliokotwa Januari 17.2026 akiwa ametelekezwa katika eneo jirani na nyumba ya wageni ya Kasulu, Nzega Mjini

Ameeleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo, alishirikiana na Jeshi la Polisi kumchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitalini kwa uchunguzi na uangalizi, huku juhudi za kumtafuta mama yake zikiendelea bila mafanikio

Rais Dkt. Samia amemkaribisha mtoto huyo katika familia yake na kuahidi kumpatia malezi, ulinzi na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo

“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya, kuliko kumtupa mtoto ni afadhali ukamkabidhi katika mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. Kila mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake” -Rais Dkt. Samia

Related Posts