Haji Manara “Yanga Walete Kocha Mpya Haraka Sana”

Haji Manara "Yanga Walete Kocha Mpya Haraka Sana"
Haji Manara “Yanga Walete Kocha Mpya Haraka Sana”

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Young Africans na Diwani wa kata ya Kariakoo, MH. Haji Sunday Manara, ameuandikia uongozi wa klabu hiyo ujumbe mzito wa tahadhari akisisitiza umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi na ya haraka kufuatia mwenendo wa sasa wa timu, huku akishauri kuwa kesho Jumatatu ingekuwa siku mwafaka kwa kocha mpya kuwasili nchini kuanza kazi.

Manara, ambaye ni shabiki lialia wa Wananchi, amebainisha kuwa kufanya maamuzi pekee haitoshi, bali yanapaswa kuwa maamuzi sahihi yanayotekelezwa kwa kasi ili kuokoa muda na kuwapa wachezaji waliopo mbinu mpya zitakazofufua makali ya timu kuelekea hatua muhimu za msimu.

Akiwa kama mdau muhimu wa soka, Manara amewasihi viongozi kutochelewa katika mchakato huo wa mabadiliko ya benchi la ufundi, akiamini kuwa kuleta mwalimu mwenye uwezo wa kuwafunda wachezaji hao kwa ufanisi ndio suluhisho pekee la kuivusha Yanga katika kipindi hiki ambacho mashabiki wanatarajia kuona timu yao ikirejea kwenye ufalme wake.

Related Posts