Waziri Gwajima Akanusha Kumzungumzia Pole Pole

Waziri Gwajima Akanusha Kumzungumzia Pole Pole
Waziri Gwajima Akanusha Kumzungumzia Pole Pole

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Mh Dorothy Gwajima amekanusha kuhusu habari iliyoandikwa juu yake akizungumzia Ndg. Humphrey Polepole akisisitiza kuwa habari hizo ni za uongo na hazina msingi wowote wa kweli.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:
“Ndugu wabaya wangu kokote mliko, nawasalimu. Naomba tusitengenezeane habari za uongo kwa malengo binafsi. Kama ni habari inayonihusu mimi, naweza kuisema mwenyewe kwenye kurasa zangu zote. Habari hii kwenye picha na maneno yaliyokuwa yameandikwa chini yake ni ya uongo, IPUUZWE.”

Waziri Gwajima ameongeza kuwa atachukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote atakayesababisha ueneaji wa taarifa zisizo sahihi:

“Nitashtaki Polisi ili walioniwekea maneno haya mdomoni watafutwe kwa mujibu wa Sheria. Sitakubali uongo, maana uongo ni ufitini na adui wa haki.”

Aidha, ameitaka jamii kutoa link au vyanzo vyote vya habari hizi ili kuchukuliwa hatua stahiki. Wakati huo huo, ameomba ushirikiano wa Polisi Tanzania kwa uchunguzi wa kina.

Waziri Gwajima anasisitiza kuwa habari sahihi kuhusu yeye zitatolewa na yeye mwenyewe, na wafuasi wake wanapaswa kutoamini posts zisizo rasmi.

Related Posts