
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema nchi hiyo ipo tayari kuwa sehemu ya vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati (Israel-Marekani dhidi ya Iran na Hezbollah) na kuwa upande wa Israel kama kutakua na mazungumzo yoyote ya kuiangamiza Israel.
“mazungumzo yoyote ya kuangamiza au kuipiga Israel yatatuingiza vitani(upande wa Israel)” amesema Muhoozi
Muhoozi ameyasema hayo leo Machi 25, 2026 kupitia chapisho lake kwenye ukurasa wa mtandao wa X akieleza kuwa wamechoshwa na vita hivyo huku akitaka visimame mara moja.
“Tunataka vita vya Mashariki ya Kati vikome sasa. Dunia imechoshwa navyo.” alisisitiza Jenerali Muhoozi ambaye ni mtoto wa Rais wa Uganada Yoweri Kaguta Museveni.
Ni mara kadhaa Muhoozi amekuwa akilitaja Jeshi la Uganda kuwa ni jeshi la Mungu huku akisema hakuna wa kupambana na Jeshi hilo. Hata hivyo matamko yake ya mtandaoni yamekuwa na ukakasi kwani mara kadhaa amechapisha na kufuta huku baadhi ya maelekezo yake kutotekelezwa na vikosi vya Uganda na mara nyingine hulazimika yeye kuomba msamaha kwa machapisho yake
