
Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City kutoka Tanzania imepoteza kwa mara ya kwanza kufuatia kipigo cha vikapu 118 kwa 97 dhidi ya Al Ahly Benghazi ya Libya kwenye Michuano ya BAL 2026, (Basketball African League)
Dar City ambayo ilishinda michezo miwili mfulululizo kabla ya kipigo cha leo imesaliwa na michezo miwili dhidi ya Petro de Luanda ya Angola Aprili 3, 2026 kabla ya kuvaana na RSSB Tigers ya Rwanda Aprili 4, 2026.
Michezo hiyo miwili inatarajiwa kuamua hatma Wawakilishi hao pekee wa Tanzania kwenye michuano hiyo inayoendelea Nchini Afrika Kusini.
