
Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania, umezumgumzia kifo cha Mwanamitandao ya kijamii kutoka Miami, Ashly Robinson (31), aliyefariki dunia April 9, 2026, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi akiwa Visiwani Zanzibar,
Kauli ya Ubalozi huo, inatokana na maswali yaliyoulizwa na AyoTV, iliyotaka kufahamu kwa kina juu ya taratibu ambazo Ubalozi huo unafanya pindi raia wa taifa lao anapofariki nje ya Marekani, ambapo Msemaji wa Ubalozi huo Nchini Tanzania amejibu kupitia barua Pepe na kusema;
“Raia wa Marekani akifariki dunia nje ya Nchi, Ubalozi wa Marekani
hutoa msaada wa Kibalozi kwa Wanasheria, mwakilishi, Jamaa wa karibu, na Familia.
“Wakati Raia wa Marekani akifariki katika Nchi ya kigeni, mamlaka za ndani wana jukumu kuchunguza chanzo cha kifo na kutoa taarifa au matokeo ya uchunguzi huo,”.
“Tunaweza kuthibitisha kifo cha Raia wa Marekani kilichotokea
Zanzibar, Tanzania tarehe 9 Aprili 2026, na tunatoa rambi rambi zetu za dhati kwa familia na wapendwa
juu ya kuondokewa kwa Ndugu yao,”.
“Kwa heshima ya faragha ya
familia na wapendwa katika wakati huu mgumu, sisi hatuna maoni zaidi.”
Katika tukio hilo, mamlaka za Zanzibar zinamshikilia mchumba wake, Joe McCann, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
