John Mnyika “Ofisi za Chadema Nchi Nzima Zifunguliwe”

John Mnyika "Ofisi za Chadema Nchi Nzima Zifunguliwe"
John Mnyika “Ofisi za Chadema Nchi Nzima Zifunguliwe”

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ametangaza rasmi kwamba kuanzia leo April 15, 2026, Ofisi za Makao Makao Makuu ya Chama hicho zimefunguliwa rasmi na kazi inaanza na amewatangazia Viongozi wa Mikoa yote kufungua Ofisi kuanzia leo hatua ambayo inakuja baada ya Mahakama ya Rufaa kukiondolea Chama hicho zuio kuanzia leo.

Akiongea na Wanahabari kwenye Makao Makuu ya Chama hicho Mikocheni Dar es salaam leo, Mnyika amesema “Ndugu Wanahabari tunawashukuru sana kwa kuitika wito wetu wa haraka haraka wa leo leo wa kuja kuzungumza na nyinyi, ni kwa mara ya kwanza toka zuio la Mahakama la June 10, 2025 ni kwa mara ya kwanza ukumbi huu unafunguliwa mlango rasmi na Mkutano na Wanahabari unafanyika, zikiwa zimepita siku 310 Makao Makuu ya Chama yakiwa yamefungwa pamoja na kuwa amri iliyotolewa tuliiona kuwa ni haramu na haikuhusu Viongozi wote lakini Watawala dhalimu wakaitafsiri kuwa inahusu Viongozi wote wa CHADEMA”

“Pamoja na kuwa amri hiyo miezi 6 ya ukomo wake ilifika December 10, 2025 lakini Watawala batili wakaendelea kutumia Vyombo vyao kusimamia amri isiyokuwa halali, sisi kama Chama kinachoheshimu utawala wa Sheria hatukutaka kuwapa Watawala dhalimu na haramu visingizio na tukafunga Makao Makuu ya Chama kwa shughuli za kiutendaji”

“Kwahiyo kwa nafasi yangu ya Mtendaji Mkuu wa Chama nitangaze kwamba Ofisi za Makao Makao Makuu ya Chama zimefunguliwa rasmi na kazi kuanzia leo zitaendelea kama kawaida, na tunawahimiza Viongozi wetu kuendelea kuzifungua ofisi za Chama na kufanya kazi kwenye maeneo yao, ofisi za Chama nchi nzima zifunguliwe rasmi na kazi za Chama za kiofisi ziendelee nchi nzima”

Related Posts