
Anaandika @kelvinrabson_
✍🏼 Simba kuanza na Chama – Maema – Kagoma na Loemba kwenye kiungo kulirahisisha kazi yao wakati wanaunda mashambilizi na kukifanikisha kufika eneo la mwisho na waliweka mtego hasa wakati Yanga wakiwa na mpira.
1: Simba walitengeneza mtengo kwenye “ Turn overs “ pale Yanga wanapoteza mpira wanaunda mashambulizi ya haraka .
2: Uwepo wa Chama kulirahisha vitu kwa Simba ( pasia mpira kwenye nafasi , maamuzi ya haraka kwenye move na alifanya move za hatari kwenda mbele ) + wachezaji wengi wa mbele wana kasi maana yake rahisi kupata nafasi eneo la mbele ( Turnovers goli la Gueye )
3: Nafikiri muundo wa ulinzi kwa Yanga wakipoteza mpira wanakuwa wazi sana ( Poor Rest Defend ) na ndio maana ilikuwa rahisi kwa Simba kufika eneo la mwisho kirahisi sana .
✍🏼 Kipindi cha pili Yanga waliboresha game yao hasa wakiwa na mpira : pasia mpira kwa usahihi kwenye nafasi , fanya uwanja kuwa mpana zaidi ( Fullbacks wa Simba kuzuia wakiwa pembeni zaidi maana yake nafasi zinafunguka eneo la ndani : Okello , Duke , Maxi wanapata nafasi kwenye mpira na spaces za kupasia mpira , Yanga wakaanza kupata nafasi kwenye defense ya Simba )
✍🏼 Baada ya hapo ni Yanga watatumiaje nafasi “ Ufanisi “ ( walitengeneza nafasi nyingi nzuri hasa kipindi cha pili na Simba walikuwa chini sana )
NOTE :
1: Chama kacheza game bora sana , hasa kipindi cha kwanza .
2: Inno Loemba kwenye kupandisha mashambulizi “ Superb “ 👍🏽
3: Ellie Mpanzu na Gueye walitoa game ngumu dhidi ya defense ya Yanga .
4: Pacome alileta uhai kwa Yanga kipindi cha pili .
5: Bakari na Bacca kushinda duels zao 🔥
6: Duke kacheza game bora kama no 6 .
7: Diarra kashinda hii Alama moja ( Saves bora kwenye game )
FT : Simba Sc 2-2 Yanga SC
MBIO ZA UBINGWA ?
Yanga – 48pts
Simba – 43pts
Azam – 40pts
Bado mechi 10
