
Global TV imefika eneo la Kitunda Kibeberu, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, ambako kichwa cha marehemu James Temba kilikutwa kikiwa kimefukiwa, tukio lililoacha simanzi na taharuki kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Akizungumza na Global TV, Aisha Juma ambaye ni Mjumbe wa Mtaa eneo hilo, amesema wananchi walipata taarifa za uwepo wa kitu kinachotiliwa shaka kabla ya kufika eneo husika na kushuhudia mabaki hayo ya mwili.
Aisha amesema baada ya uchunguzi wa awali kufanyika, ilibainika kuwa ni kichwa cha binadamu kilichokuwa kimefukiwa ardhini, hali iliyowalazimu kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.
Marehemu James Temba
“Tulipopata taarifa tulifika eneo la tukio na kukuta kweli kuna mabaki yaliyokuwa yamefukiwa. Polisi walifika muda mfupi baadaye kwa ajili ya uchunguzi,” amesema Aisha.
Tukio hilo limezua hofu kwa baadhi ya wakazi wa Kitunda Kibeberu huku wengi wakitaka uchunguzi wa haraka kufanyika ili kubaini waliohusika na tukio hilo pamoja na chanzo chake.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku wananchi wakihimizwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka pale wanapokuwa na taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi.
VIDEO:
